kipi kipya?

Imeboreshwa kutanua toleo la msaada 102

Usomaji wa picha "toleo la msaada la upanuzi wa Firefox 102"]

hivyo, wakati umefika wa kuboresha Kivinjari cha Tor Browser kwa toleo jipya la Msaada wa Firefox wa Muda mrefu. Tumetumia miezi michache iliyopita tangu kutolewa kwa Tor Browser11.5 kupitia hati ya kutolewa ya ESR 102 ili kuhakikisha kila mabadiliko ni yanafaa na Kivinjari cha Tor Browser. Kama sehemu ya mchakato huo, chochote ambacho kinaweza kupingana na kanuni kali za faragha na ulinzi wa Tor Browser huwa zinalemazwa kwa uangalifu.

Msaada wa lugha nyingi kwa desktop

Kielelezo cha menyu hutumika kuchagua lugha ya kuonyesha ya Tor Browser 12.0

Awali, ikiwa ulitaka kutumia Tor Browserbkwenye kompyuta yenye lugha nyingine zaidi ya Kiingereza, ulihitaji kutafuta na kupakua mojawapo ya toleo la lugha linalolingana kutoka kwenye ukurasa wetu wa kupakua. Kubadili lugha baada ya kusakinisha Tor Browser haikuwa kazi rahisi, na inahitaji kuongeza kifurushi kipya ya lugha kwenye usakinishaji wako wa sasa, au kupakua upya Tor Browser kutoka mwanzo.

Hadi leo tunafurahi kutangaza kwamba hili ni jambo la zamani: Tor Browser ya desktop sasa inalugha nyingi, maana yake ni lugha zote za msaada sasa zimejumuishwa katika kifungu kimoja. Kwa watumiaji wapya, Kivinjari cha TorBrowser 12.0 kitasasisha yenyewe moja kwa moja unapokianzisha ili kulingana na lugha ya mfumo wako. Na kama umejiboresha kwenye Tor Browser 11.5.8, browser itajaribu kudumisha lugha yako ya kuonyesha uliyoichagua awali.

Kwa njia yoyote, sasa unaweza kubadili lugha ya kuonyesha bila kupakua chochote zaidi kupitia menyu ya Lugha katika mipangilio ya Jumla - lakini bado tunapendekeza kuanza upya kwa haraka kivinjari cha Tor Browser kabla ya mabadiliko hayajaanza kutumika kabisa.

kiuhalisia kuunganisha lugha nyingi katika kupakua moja kunapaswa kuongeza ukubwa wa faili ya kivinjari cha Tor Browser - tunafahamu sana hili; hata hivyo, tumepata njia ya kuokoa ufanisi mahali pengine, hivyo tofauti ya ukubwa wa faili kati ya Kivinjari cha Tor Browser 11.5 na 12.0 ni ndogo.

Msaada wa silikoni wa asili ya Apple

Apple Silicon logo

hii haikuwa zoezi dogo, lakini tunafuraha kusema kuwa Tor Browser 12.0 kwa sasa inasaidia Apple Silicon natively. Kama njia ya Mozilla kwa Firefox, tumechagua la Universal Binary pia - maana yake, toleo la x86-64 (yaani Intel inayofaa) na ARM64 (yaani Apple Silicon inayofaa) zinajumuishwa pamoja na toleo sahihi kuchaguliwa moja kwa moja wakati wa kukimbia.

HTTPS- ni kwa chaguo msingi tu kwa Android

Usomaji wa picha "hali pekee ya HTTPS" na Switch huwashwa

Hapo Julai, tulisambaza taarifa kuhusu Tor Browser kwa watumjia wa Android na watarajiwa wetu wa hivi karibuni katika toleo la Tor Browser 11.5 release post. Tangu mwanzo wa mwaka huu, wabunifu wetu wamekuwa wakifanya kazi kwa bidii ili kuendelea na sasisho za kawaida kwa Android, kuboresha utulivu wa programu, na kufikia mzunguko wa kutolewa kwa Fenix (Firefox kwa Android).

Awamu inayofuata katika mpango wetu wa Android ni kuanza kuhamisha vipengele vilivyochaguliwa na vyenye kipaumbele cha juu ambavyo vilitolewa hivi karibuni kwenye desktop na kuwapeleka kwenye Android - kuanzia na kuwezesha Mode ya HTTPS-Only kwa chaguo-msingi. Mabadiliko haya yatasaidia kutoa kiwango sawa cha ulinzi dhidi ya mashambulizi ya SSL kwa njia mbaya za kutoea relay ambazo tulizianzisha kwenye desktop katika Tor Browser 11.5.

Weka kipaumbele. tovuti za onion kwenye Android

Kielelezo cha kuchagua kipaumbele cha tovuti za onion katika Tor Browser kwenye faragha na ulinzi wa mpangilio wa skrini wa Android

Nyingine ndogo lakini inaweza ikaboresha kwenye Tor Browser 12.0 katika Android ni chaguo "kuweka kipaumbele. tovuti za onion" ambako zinapatikana. Unapo wezeshwa, utaongozwa moja kwa moja kwenye tovuti ya onion iliyolinganishwa na tovuti yeyote yenye eneo la onion iliyosanidiwa- kukusaidia kugundua tovuti mpya za onion katika mfumo.

Unaweza kugeuza "kuweka kipaumbele cha tovuti za onion" chini ya kipengele cha faragha na ulinzi ndani ya Tor Browser katika mpangilio wa menyu ya Android. Tafadhali fahamu kuwa sasisho hili halijumuishi kifungo cha ".onion available" cha rangi ya zambarau katika kisanduku cha anwani, ambacho bado ni cha pekee kwa kivinjari cha TorBrowser kwa kompyuta ya mezani.

Na zaidi...

12.0 ni toleo la kwanza la Tor Browser ambalo husaidia Kialbeni (sq) na Kiukreni (uk). Tunatoa shukrani kubwa kwa wote waliotoa muda wao kujitolea na kufanya kazi kwa bidii katika kutafsiri Tor Browser katika lugha mbalimbali <3

Ikiwa utaona neno ambalo bado linahitaji kutafsiriwa, au ungependa kuchangia katika localizationya lugha nyingine, tafadhali tembelea kituo chetu cha jamii ili kujua jinsi ya kuanza.

Tumekuwa na shughuli nyingi pia za kufanya uboreshaji mbalimbali nyuma ya pazia kwenye vipengele kama tor-launcher (ambayo huanzisha tor ndani ya Tor Browser), ambayo msimbo umepitia marekebisho makubwa. Hivyo, kama unatumia muundo wa Tor Browser usio wa kawaida (kama kutumia mfumo wa tor kujiunganisha na Tor Browser, au mpangilio maalum wa mtandao) na utapata ujumbe wa dosari usioutarajia wakati wa uzinduzi wa Tor- tafadhali tujulishe kwa kujaza tatizo hilo kwenye ripoti yetu ya Gitlab.

mwisho, Tor Browser kipengele cha letterboxingkimeboreshwa kidogo katika uzoefu wa mtumiaji, ikiwa ni pamoja na (lakini sio mdogo kwa) kurekebisha uvujaji na njia za kuepuka, kuondoa mpaka wa 1px katika video za skrini kamili, na kulemaza kipengele kikamilifu kwenye kurasa zinazohusiana na Tor zilizoaminika kama skrini ya Kuunganisha kwenye Tor, miongoni mwa mambo mengine.

tuma mrejesho yako

Ikiwa una mapendekezo juu ya jinsi tunavyoweza kuboresha toleo hili, tafadhali tujulishe. Asante kwa timu zote katika Tor, na kwa wale wengi waliojitolea, ambao wamechangia kwa toleo hili.

Unaitaji msaada?

Angalia FAQ katika jamii yetu

Tembelea Msaada

Wasiliana

wasiliana na sisi moja kwa moja!

Jiunge nasi kwenye IRC