mgawanyo wa msaada kutoka katika faragha ya mtumiaji na faragha mtandaoni

_tuzo za _Cy pres ni fedha zinazotolewa kama sehemu ya makazi ya kesi ya matabaka nchini Marekani. Wakati fedha zote haziwezi kutolewa kwa wanachama wa madaraja , zinaweza kutolewa kwa mashirika yasiyo ya faida, ya utetezi, na ya utafiti ambayo kwa ujumla wanawakilisha wanachama wa madaraja. Cy pres tuzo za faragha ya watumiaji zinaweza kusaidia mradi wa Tor kuelimisha watu binafsi na mashirika kuhusu jinsi ya kudumisha faragha yao mtandaoni, kuhamasisha ulinzi wa faragha, na kujenga teknolojia muhimu huru na chanzo wazi ambazo zinaipa kipaumbele faragha.

kuhusu Tor Project

Tor Projeect inapatikana U.S 501(c)3 ni shirika lisilo la serikali lililogunduliwa mwaka 2006 kwa lengo la kuimarisha haki za binadamu pamoja na uhuru:

  • kuunda na kusambaza teknolojia za uhuru na faragha bila malipo na zisizo na mipaka ya utambulisho,
  • kusaidia upatikanajinwa matumizi yao bila kikwazo, na
  • kukuza ufahamu wao wa kisayansi na maarufu zaidi.

Tor project na jamii inayozunguka inaweza kusambaza inayotumika zaidi bure , vyanzo vya wazi vya teknolojia: Tor Browser na mtandao wa Tor.

pamoja na kuendeleza teknolojia, shirika linasaidia watu kuweza kulinda faragha zao mtandaoni. Tor project umewafundisha maelfu ya wanaharakati, waandishi wa habari, na wapigania haki za binadamu, maktaba ,watumiaji wa mtandao wa kawaida jinsi ya kulinda na kudumisha faragha mtandaoni.

Tor project imetambuliwa kuwa ndio mtaalamu zaidi kwenye mtandao wa faragha. na imebadilishwa na vyombo vya habari kuonyesha jinsi watu binafsi na watumiaji wanaweza kutunza faragha zao mtandaoni.

Katika siku za nyuma, Tor Project umepokea tuzo za cy pres za faragha ya watumiaji kupitia ruzuku za faragha ya watumiaji za Rose Foundation. Shirika hilo lina uzoefu wa zaidi ya muongo mmoja wa kufanikiwa kutekeleza miradi na wafadhili na washirika mbalimbali kama Idara ya Serikali ya Marekani - Ofisi ya Kidemokrasia, Haki za Binadamu, na Kazi; Shirika la Kitaifa la Sayansi; Wakala wa Miradi ya Utafiti ya usalama (DARPA); na msaada wa vyombo vya habari kidemokrasia.

wasiliana na Tor Project kuhusu mgawanyo wa msaada

Kama ungependa kuongea na mtu kutoka kwenye Tor project kuhusu kama shirika linaweza kuwa sahihi kwa tuzo ya cy pres tafadhali, wasiliana na timu kwa barua pepe grants@torproject.org.

kusoma zaidi