PrivChat

Mjadala kuhusiana na teknolojia, haki za binadamu,
na uhuru wa mtandao umeletwa kwako na Tor Project

PrivChat ni mfululizo wa matukio ya harambee yaliyofanywa kuchangia Tor Project. Kupitia PrivChat, tutakuletea taarifa muhimu kuhusiana na nini kinaendelea katika teknolojia, haki za binadamu, na uhuru wa mtandao kwa kukusanya wataalamu wabobezi kuwasilana kwa majibinazo na jamii yetu.


Sura ya #2- Nzuri, Mbaya na Mbaya kwa ukwepaji wa udhibiti

Angalia

Kila mwaka, udhibiti wa mtandao unaongezeka ulimwenguni.Kutoka katika kiwango cha udhibiti wa mtandao hadi udhibiti wa mtandao kitaifa, serikali na makampuni binafsi wana zana zenye nguvu kuzuia taarifa na mawasiliano kwa watu. Watu wengi, makundi na taasisi wanafanya kazi ya uvumbuzi, kupima na kupambana dhidi ya udhibiti wa mtandao-- na wanawasaidia mamilioni ya watu kujiunganisha na mtandao mara kwa mara na kwa usalama. Licha ya mafanikio hayo, tunapitia changamoto ya kutopata ufadhili mzuri mabilioni ya dola kutumia katika udhibiti na mbinu nyingine zikiendelea. Toleo la pili la PrivChat la Tor linaweza kuhusu uzuri, ubaya unaotokea katika ukwepaji wa udhibiti wa mtandao. Katika dunia ambayo teknolojia ya udhibiti unazidi kuwa wa kisasa na inanunuliwa na kuuzwa katika nchi, hivyo ni ubunifu wetu kupima na kutengeneza dhana za kukwepa udhibiti huo, vilevile na utayari wa watu kupambana na hilo. Lakini je inatosha? Vikwazo gani vinawapata watu na taasisi wanapopambania uhuru wao wa mtandao?

Mtunzaji

Cory Doctorow

Electronic Frontier Foundation, MIT

Cory Doctorow Ni mtunzi wa liwaya za sayansi, mwanaharakati, na mwanahabari. Ni mtunzi wa RADICALIZED na WALKAWAY, Liwaya za sayansi kwa watu wazima, kitabu cha picha cha YA kinachoitwa IN REAL LIFE, kitabu cha biashara INFORMATION DOESN’T WANT TO BE FREE, na vitabu vya vijana wadogo kama HOMELAND, PIRATE CINEMA and LITTLE BROTHER. Kitabu chake cha hivi karibuni ni POESY THE MONSTER SLAYER, kitabu cha picha kwa viongozi wadogo. Kitabu chake kifuatacho ni ATTACK SURFACE, na cha watu wazima LITTLE BROTHER. Ameimarisha blogi yake ya kila siku ya Pluralistic.net. Anafanya kazi na Electronic Frontier Foundation, ni mtafiti katika maabara ya MT Media Lab Research, ni profesa mtembeleaji katika Chuo Huria cha Computer Science, profesa mtembeleaji katika Chuo kikuu cha North Carolina’s School of Library and Information Science na mwanzilishi mwenza wa UK Open Rights Group. Alizaliwain Toronto, Canada, kwa sasa anaishi Los Angeles.

Washiriki

Felicia Anthonio

Mwanakampenikiongozi katika Access Now, #KeepItOn

Felicia Anthonio anafanya kazi na Access Now kama Mwanakampeni ya #KeepItOn, kampeni ya dunia inayopinga kuzimwa kwa mtandao. Muungano wa #KeepItOn unaundwa na zaidi ya taasisi 210 duniani kote. Kabla ya kujiunga na Access Now, alikuwa Programme Associate wa Media Foundation ya West Africa (MFWA) ambapo aliratibu African Freedom of Expression Exchange (AFEX), mtandao wa kibara ambao wa taasisi za uhuru wa kujielezea barani Africa. Felicia led the AFEX’s anafanya kampeni na uchechemuzi katika uhuru wa kujielezea ikihusisha usalama wa wanahabari, ufikiwaji wa habari na uhuru wa mtandao na haki za kidigitali zikiwa zinalenga kuboresha sera ambazo haziruhusu uhuru wa kujielezea (nje ya mtandao na mtandaoni). Ni mshirika katika programu ya African Internet Governance School (AfriSIG ya mwaka 2019). Nana shahada ya uzamili katika Lettres, Langues et Affaires Internationales Kutoka chuo kikuu chal’ Université d’Orléans, Ufaransa na ana shahada ya sanaa katikia French and Psychology kutoka chuo kikuu cha Ghana.

Vrinda Bhandari

Katika ushauri - Litigation, Internet Freedom Foundation

Vrinda Bhandari ni mwanasheria anayechukua hatua za kisheria wa New Delhi, India, na amebobea katika mambo ya haki za kidigitali, teknolojia,na faragha. Amekuwa akijihusisha katika kuchukua hatua za kisheria juu ya mambo ya kibayometriki nchini India (Aadhaar), Programu ya kuchukua mawasiliano iliyotengenezwa na serikali (Aarogya Setu), kurudisha mtandao Jammu & Kashmir, na changamoto za sheria za nchi juu ya ufuatikliaji mtandaoni na kashfa za jinai zinazotokea nchini India. Vrinda pia ameshauri na kuwakilisha watumiaji katika maswala yanayohusiana na uzuiliwaji wa tovuti, kasha na uchochezi. Vrinda ni mwanafunzi wa Rhodes Scholar, aliyehitimu kutoka Chuo kikuu cha Oxford katika shahada ya uzamili ya Sheria (BCL) na shahada ya uzamivu katika Public Policy (MPP), na akapokea shahada yake ya kwanza kutoka National Law School ya Chuo kikuu cha India, Bangalore.

Cecylia Bocovich

Mtengenezaji, Tor Project

Cecylia ni mtengenezaji wa programu katika at Tor Project ambapo analenga kutengeneza vifaa vya kukwepa udhibiti na kuwawezesha watumiaji wote kuupata mtandao wa Tor. Ni muhitimu kutoka chuo kikuu cha Waterloo na shahada ya uzamivu katika Computer Science mwaka 2018, na kuendelea kushiriki katika Kritoprografia, Usalama na Faragha (CrySP) katika maabara ya utafiti kama mtafiti mtembeleaji. Kama mwanafunzi muhitimu, amefanya utafiti wa mbinu za kukwepa udhibiti ambazo zinakinzana na mashine kubwa zenye nguvu ya kuzuia, pia matumizi ya vifaa vya faragha. Kwa sasa anatumika kama mkurugenzi mshauri wa Open Privacy, taasisi isiyoingiza faida inayofanya kazi ya kuendeleza teknolojia za faragha ambazo zinawezesha jamii na kuwezesha utayari. Pia alisaidia kuanzisha, kupanga na kwa sasa anatumika kama mwenyekiti wa kamati ya utafiti wa jarida linaloendelea la Privacy Enhancing Technologies (PoPETs), kwa lengo la kusaidia na kukuza usambazaji wa vyanzo vya data za utafiti wa faragha katika jamii.

Arturo Filastò

Mhandisi na Kiongzoai wa, OONI

Arturo mwanzilishi mwenza wa Open Observatory of Network Interference (OONI) mwaka 2011 na tangia hapo ametumika kama kiongozi wa mradi wake na muhandisi mwenza. Kwa mara ya kwanza alifanya kazi na Tor Project kama mtengenezaji na aliunda programu zibgine kadhaa zinazokuza haki za kibinadamu, kama vile GlobaLeaks. Pia ni muanzilishi mwenza na anafanya kama makamu wa raisi wa Hermes Center for Digital Human Rights. Arturo amesoma Mathematics and Computer Science katika chuo kikuu cha Roma “La Sapienza”.

Mchango wako unafanya mfululizo huu na kazi zetu katika Tor kuwezekana.

Njia bora ya kuunga mkono kazi zetu ni kuwa mchangiaji wa kila mwezi.