PrivChat

Mjadala kuhusiana na teknolojia, haki za binadamu,
na uhuru wa mtandao umeletwa kwako na Tor Project

PrivChat ni mfululizo wa matukio ya harambee yaliyofanywa kuchangia Tor Project. Kupitia PrivChat, tutakuletea taarifa muhimu kuhusiana na nini kinaendelea katika teknolojia, haki za binadamu, na uhuru wa mtandao kwa kukusanya wataalamu wabobezi kuwasilana kwa majibinazo na jamii yetu.


Sura ya #3-Tor kuendeleza haki za binadamu

Angalia

Dhima kuu ya Tor Project's ni kukuza haki za kibinadamu na uhuru kwa kuunda na kueneza teknolojia huru, za bure na za wazi na faragha na usiri mtandaoni. Watu wanatumia teknolojia yetu, inayoitwa mtandao wa Tor na Tor Browser, kwa njia tofauti. Tor inatumika na watoa taarifa wanaohitaji njia salama kuleta taarifa nzuri za matendo mabaya -- taarifa hizi ni muhimu jamii kujua -- bila kujulikana wao ni nani. Tor inatumika na wanaharakati duniani kote ambao wanapinga serikani kandanizi na kulinda haki za binadamu, sio tu kwa usalama wao na kutojulikana, lakini pia kukwepa udhibiti wa mtandao ili sauti zao zisikike. Tor inawezesha mamilioni ya watu kujilinda mtandaoni, Haijalishi nafasi walizonazo au wasizonazo. Kwa toleo letu la tatu la PrivChat, tutaleta maisha halisi ya watumiaji wa Tor ambao wataelezea namna Tor imekuwa muhimu kwao na kazi zao katika kulinda haki za binadamu na uhuru duniani kote.

Mtunzaji

Edward Snowden

Raisi, Freedom of the Press Foundation

Edward Snowden ni raia wa Marekani, afisa intelijensia na mtoa habari aliyepita. Nyaraka alizoweka wazi imetoa ukurasa muhimu kwa umma katika NSA na washirika wenza wa kimataifa wa intelijensia’ programu nyingi za siri za ufuatiliaji na uwezo. Taarifa hizi umetengeneza umakini mkubwa sana duniani kote katika kuingilia faragha na usalama wa kidigitali na usalama wa kidigitali, ikapalekea mjadala wa kidunia juu ya maswala hayo.

Washiriki

Alison Macrina

Muanzilishi wa , Library Freedom Project

Alison Macrina ni mkutubi na muanzilishi wa mradi wa Library Freedom, utendani wa jamii ya wafanya kazi wa maktaba kuishi katika misingi yetu ya uhuru wa taaluma na faragha katika ulimwengu halisi. Kazi yake ililenga katika kuangalia madhara ya ufuatiliwaji katika jamii ya wakutubi na kazi za wakutubi, namna ufuatiliaji unahusiana na maswala mengine ya haki za kijamii na uhuru wa taaluma, na nguvu ya mabadiliko katika teknolojia zetu. Alison na mradi wa Library Freedom wamepata tuzo ya Free Software Foundation's kwa mradi wa Social Benefit, Library Journal's Movers na Shakers, tuzo ya the New York Library Association's Intellectual Freedom, nna tuzo ya LITA/Library Hi Tech .

Berhan Taye

Meneja wa Sera za Afrika na kuongoza kuzima mtandao duniani, Access Now

Berhan Taye (She/her) ni mtafiti anayechunguza uhusiano uliopo kati ya teknolojia, jamii, na haki za kijamii. Ni meneja wa Africa Policy na kiongozi wa Global Internet Shutdowns katika taasisi ya Access Now. Ameongoza kampeni ya #KeepItOn, kampeni ya dunia ya kuzuia vitendo vya uzimwaji wa mtandao kwa muungano wa zaidi ya mashirika wanachama 220 duniani kote. Kabla hajajiunga na Access Now, alikuwa mtafiti wa mambo ya teknolojia kwa ajili ya haki za kijamii mradi wa ukaguzi ambao umetoa taarifa ya MoreThanCode.cc.

Ramy Raoof

Mwanateknolojia wa Maabara ya Usalama, Amnesty International

Ramy Raoof ni mtafiti wa teknolojia na faragha, kazi zake za hivi karibuni zimelenga katika kufanya tafiti za mashambulio ya kidigitalki yaliyokusudiwa kinyume na wapigania haki za binadamu ma ,mashirika yasiyo ya kiserikali na kuendeleza taratibu za ulinzi wa kidigitali na kuwajengea uwezo wanaharakati katika nchi za mashariki ya kati na Marekani ya kati kuhusiana na ufuatiliaji mtandaoni na udhibiti. Ramy ni mwanateknolojia anayechunguza na kuangalia madhara ya teknolojia katika jamii katika maabara ya Amnesty International's Security na pia yupo katika Tor Project kama mjumbe wa bodi ya wakurugenzi. Kabla hajajiunga na Amnesty, alitumika kama mwanateknolojia mkuu katikaEgyptian Initiative for Personal Rights (EIPR). Ramy amepokea tuzo ya kimataifa ya Heroes of Human Rights na Communications Surveillance kutoka kwa Access Now mwaka 2017 na mwezi Mei 2016 alipokea tuzo ya kimataifa ya international Bobs - Best of Online Activism kama njia ya kutaambua mchango wake katika usalama wa kidigitali na faragha kutoka kwa Deutsche Welle. Katika Twitter https://twitter.com/RamyRaoof.

Mchango wako unafanya mfululizo huu na kazi zetu katika Tor kuwezekana.

Njia bora ya kuunga mkono kazi zetu ni kuwa mchangiaji wa kila mwezi.