Hii ni toleo la kwanza la uthabiti linalotegemea Firefox ESR 91, na linajumuisha sasisho muhimu la Tor 0.4.6.8.
kipi kipya?
Tor Browser inapata mtazamo mpya
Mapema mwaka huu, kitumizi cha Firefox kiliwekwa upya kwa lengo la kuifanya kivinjari kiwe rahisi kutumia, kupunguza orodha za menyu na kuwa na muundo mpya kabisa wa kurasa.
Firefox ESR 91 imetambulisha muundo mpya kwa Tor Browser kwa mara ya kwanza.
Ili kuhakikisha inakidhi uzoefu mpya, kila kipengee cha UI iliyobinafsishwa katika Tor Browser kimeboreshwa kuendana na muonekano mpya wa Firefox.
hivyo inajumuisha kila kitu kutoka kusasishwa kwa vitu vya msingi kama rangi, uchapaji na vitufe hadi kuchora upya alama zetu zote ili ziendane na mtindo mpya wa alama nyembamba.
Nje ya kivinjari chenyewe cha chrome, skrini ya uunganisho, onyesho la circuit, viwango vya usalama na makosa ya tovuti ya onion vyote vilipata uboreshaji - vikiwa na marekebisho madogo lakini yenye ubora mzuri wa maisha kwa kila kimoja.
mwisho wa kutumia huduma ya onion services
Mwaka uliopita tulitangaza kwamba v2 onion services zitapitwa na wakati mwishoni mwa 2021, and since its 10.5 release Tor Browser kimekuwa kikiwaonya watumiaji wanaotembelea tovuti za onion v2 kuhusu kustaafu kwao karibuni. Hatimaye, siku hiyo imefika.
tangu kusasishwa kwa Tor 0.4.6.8 v2 onion services hazipatikani tena kwenye Tor Browser, na watumiaje wake watapokea "invalid Onion Address" badala ya dosari.
Ukipokea kosa hili unapojaribu kutembelea anwani ya v2 ambayo awali ilifanya kazi, hakuna makosa kwenye kivinjari chako - badala yake, tatizo linapatikana kwenye tovuti yenyewe.
kama utapenda, unaweza kumtaarifu msimamizi mkuu kuhusu tatizo na kumhimiza kuboresha v3 onion services haraka iwezekanavyo.
Ni rahisi kubaini kama bado una anwani za zamani za v2 zilizohifadhiwa kwenye vivinjari vyako ambavyo vinahitaji kuondolewa au kusasishwa pia: ingawa zote mbili zinaisha na .onion, anwani za v3 zenye usalama zaidi ni urefu wa herufi 56 ikilinganishwa na urefu wa v2 wa herufi 16 tu.
masuala yanayojulikana
Tor Browser 11.0 inakuja na matatizo kadhaa yanayojulikana:
- Bug 40668: DocumentFreezer & file scheme
- Bug 40671: herufi haionyeshi
- Bug 40679: Vipengele vya kupotea kwenye uzinduzi wa mara ya kwanza kwenye esr91 kwenye MacOS
- Bug 40689:badilisha Blockchair tafuta mtoaji wa HTTP method
- Bug 40667: video za AVI zinaonyesha faili lililoharibika kwenye window 111
- Kosa 40677: Tangu sasisho hadi 11.0a9 baadhi ya vifaa vya nyongeza havifanyi kazi na vinahitaji kufungwa na kufunguliwa upya kila mara unapoanza
- Tatizo 40666: Kuwaasha mipangilio ya kuzima svg.disable affects NoScript
- Bug 40690:Kivinjari cha wavuti kinaharibika wakati mode ya kuvinjari kwa faragha inapozimwa
- Kosa 40693: Utegemezi wa Wayland unaoweza kutokea
- Bug 40692: Picha imewezeshwa kwa tbb 11.0a10b (mpya)
- Bug 40700: Wezesha mapendekezo ya Firefox kuwa yamezimwa kwa chaguo-msingi (kupya)
- Bug 40705: "tembelea tovuti yetu" katika kuhusu:tbupdate kinachoelekeza sehemu tofauti (muhimu)"
- Bug 40706: Fix issue in https-e wasm (mpya)
toa mrejesho
Ikiwa una mapendekezo juu ya jinsi tunavyoweza kuboresha toleo hili, tafadhali tujulishe.
Asante kwa timu zote katika Tor, na kwa wale wengi waliojitolea, ambao wamechangia kwa toleo hili.